
Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amewashauri viongozi wa
Kenya kuheshimu wananchi ili kupata heshima sawia.
Akihutubu katika kaunti ya Embu wakati wa kusimikwa
kwa askofu Peter Ndung’u kusimamia jimbo la kanisa Katoliki Embu, Kenyatta
alisema kwamba ili Kenya kupata maendeleo na kusonga mbele, inahitaji viongozi
ambao watawaheshimu wananchi wake.
Aliwataka Wakenya wote kuungana na kuombea taifa,
akisisitiza haja ya kukomeshwa kwa siasa za kikabila.
“Tuombee
nchi yetu, tuombee Amani na uwiano kati ya viongozi na wananchi. Tuache mambo
ya ukaabila na tupendane. Sisi wote ni Wakenya na Kenya haiwezi kufaulu watu
wakiwa na utengano, wakiwa wanatupiana maneno bila kuheshimiana.”
“Viongozi
heshimu wananchi na wao watarudisha hiyo heshima,”
Kenyatta alisema.
Kiongozi huyo mstaafu alitania akisema kwamba yeye
siku hizi hana maneno mengi bali husikiza redio na kutazama runinga tu.
“Unajua
mimi siku hizi sina stori mingi, mimi huwa naangalia tu TV na kusikiliza redio,”
aliongeza.
Rais mstaafu alimuahidi askofu mpya kwamba yeye
wakati atamualika katika ibada ya kuchanga pesa kwa ujenzi wa kanisa,
hatopeleka siasa kanisani bali lake litakuwa tu lile aliloitiwa.
“Nakuhakikishia
mimi sitaleta siasa kanisani lakini nitakuja kwa yale tu uliyoniitia, kujenga
kanisa la Mungu. Kwa hivyo wakati wowote, jisikie huru kutukaribisha,”
Kenyatta alimaliza.
Mkutano huo wa kidini uliofanyika Jumamosi uliluwa wa
kwanza kwa Rais Ruto kukutana ana kwa ana na aliyekuwa naibu wake Rigathi
Gachagua ambaye alibanduliwa ofisini mwezi mmoja uliopita.
Ulikuwa ni mkutano ambao uliwakutanisha pia na rais mstaafu
Uhuru Kenyatta katika eneo la Mlima Kenya kwa mara ya kwanza tangu alipochukua
madaraka kutoka kwake mwezi Septremba 2022.
Hata hivyo, licha ya viongozi kupewa nafasi ya
kuzungumza, Gachagua hakuweza kuzungumza.
Picha zake akitembea kwenye matope kuelekea kwenye
ukumbi mkuu ziliizua mjadala mkuu kwenye mitandao ya kijamii ambapo aliketi
mbali na viongozi wengine.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!