
Aliyekuwa naibu rais, Rigathi Gachagua amewakosoa
baadhi ya wandani wa rais Ruto kwa kile alisema ni kuwashambulia viongozi wa
kanisa.
Akizungumza katika ibada ya kanisa huko Kajiado,
Gachagua alisema kwamba alisikitishwa sana kuona makumi ya wandani wa Ruto
wakiwashambulia maaskofu wa Katoliki baada ya kutoa taarifa ya kuikosoa
serikali kwa utendaji wake mbaya.
Gachagua aliwashauri viongozi hao kuwaheshimu
viongozi wa kanisa, akisema kwamba wao ndio wanajumuika na wananchi wa kawaida
karibia kila siku.
DP huyo wa zamani alisema kuwa wanachosema viongozi
wa makanisa kinafaa kutiliwa maanani kwani wao ndio wako na mwananchi wa
kawaida muda wote.
“Kama
kuna viongozi wanaofanya public participation kila siku ni viongozi wa kidini
kwa sababu wako na waumini kila siku, kila wikendi. Na kama kuna watu wanaojua
chenye ground inasema, ni viongozi wetu wa kanisa. Kwa hivyo, ukisikia viongozi
wetu wanasema kitu, tuwasikilize na tuwaheshimu,”
Gachagua alisema.
“Tulisikitishwa
sana wakati viongozi wetu wa kanisa Katoliki walipozungumza na tuliona baadhi
ya wabunge wakiwatukana, wakiwazomea na kudharau baba zetu wa Imani.”
“Wale
ni wapakwa mafuta wa Mungu, na ni sharti tuwaheshimu,”
Gachagua aliongeza.
Kiongozi huyo wa zamani hata hivyo alimpongeza rais
Ruto kwa kuzungumzia suala hilo Jumamosi katika ibada ya kusimikwa kwa padre
Peter Ndung’u kama askofu mpya wa jimbo la Katoliki Embu.
“Na nina furaha kwamba jana rais wetu Dkt William
Ruto alitambua kwamba maaskofu wa Katoliki waliibua masuala fulani na alisema
kwamba watasikilishwa au kupewa nafasi ya kujieleza. Huo ndio mkondo salama wa
kufuata.”
“Tungependa kuwaambia wale waheshimuwa wengine
waliowatukana maaskofu wa Katoliki, achene kiburi,” Gachagua alisema.
Alhamisi wiki jana, baraza la maaskofu wa kanisa
Katoliki nchini lilifanya mkutano na waandishi wa habari na kuituhumu serikali
ya William Ruto katika kile walichosema kuwa ni utendakazi mbaya.
Maaskofu hao walimsuta Ruto wakidai kwamba uongozi
wake umefanya kuwa kawaida itikadi za kudanganya pamoja na ongezeko la ufisadi
nchini.
Walimtaka rais kusikiliza vilio vya mwananchi wa
kawaida, wakisema kwamba idadi kubwa ya Wakenya hawajafurahishwa na uongozi
wake, miaka 2 tangu alipochukua uongozi wa taifa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!