Mwanaharakati na mwanasiasa Morara Kebaso ameweka wazi kwamba hatojiunga na chama au muungano wowote wa kisiasa humu nchini.

Mwanzilishi huyo wa chama cha INJECT aliwahakikishia wafuasi wake kwenye ukurasa wake wa jukwaa la X kwamba hatoyumbishwa na vuguvugu linaloendelea la kuwachukua vijana wote wa Gen Z katika vyama vikuu vya kisiasa nchini.

“Kuna jitihada kubwa sana za kuwameza viongozi wote wa GenZ kwenye vyama vya siasa vya kawaida ili kuwafundisha mtindo wa kifisadi wa zamani. Ndio maana tukaanzisha Chama cha INJECT. Tutapanga njia yetu wenyewe. Sitajiunga na UDA au ODM au WIPER muda wao umekwisha. Ni wakati wetu sasa. Uthabiti hadi mwisho,” Kebaso alisema.

Mwanaharakati huyo wa elimu ya kiraia katika sasisho jingine, alifichua kwamba upo mpango wa kuingia katika ikulu japo hakusema ni lini.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kebaso aliwataka wanachama wake wote na vijana wote kujiweka tayarikusafiri kuingia jijini Nairobi muda wowote, akidokeza kwamba kutakuna na vuguvugu kuu la kuingia kaitka ikulu ya Nairobi.

Alisisitiza kwamba mchakato huo hautakuwa rahisi kwa watu waoga, akisema kwamba kila kijana anastahili kufungia woga wake kwenye sanduku kabla ya kusafiri kuja Nairobi.

“Anza kujitayarisha. Tunaandamana hadi Ikulu hivi karibuni. Jitayarishe kusafiri kutoka kila mahali nchini Kenya hadi Nairobi. Jitayarishe kupiga kambi mjini. Tuna mgawo wa pekee unaohitaji watu wasio na woga. Chukua hofu yako na uifunge kwenye sanduku na kufuli mbili. TUNAKUHITAJI USIOGOPE. Jitayarishe na usubiri ishara,” Kebaso alisema.