
Mtahiniwa wa kike katika shule ya upili ya wasichana
ya Sironga ameripotiwa kuzirai katika chumba cha mtihani baada ya kudaiwa
kushambuliwa kwa makofi na afisa wa kulinda mtihani unaoendelea wa KCSE.
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Afisa huyo wa
uhakiki wa ubora anasemekana kuzuru shule hiyo ya kitaifa Jumanne asubuhi ili
kutathmini maendeleo ya majaribio yanayoendelea.
Alipokuwa akiingia kwenye chumba kimoja cha mtihani,
aliona mtahiniwa akitafuna kitu ambacho alishuku kuwa hakikuidhinishwa katika
chumba cha mtihani.
Kulingana na ripoti ya polisi, afisa huyo alisonga
alipokuwa mtahiniwa huyo na kumshukia kwa makofi kadhaa kabla ya kuondoka
shuleni.
Kufuatia kupigwa kofi, mtahiniwa huyo alibaki bila
utulivu alipokuwa akifanya karatasi yake ya asubuhi kabla ya kuanguka kwenye
chumba cha mtihani.
Alikimbizwa katika zahanati ya shule, ambapo hali
yake ilikuwa ikiendelea.
"Uchunguzi wa tukio hilo umeanza na maelezo
zaidi yatafuata," ilisoma sehemu ya ripoti ya polisi.
“Ni makosa kumshambulia mtu. Mwanafunzi tayari
amejaza fomu ya P3. Tutategemea walioshuhudia tukio hilo na ikiwa kuna ushahidi
wa kutosha, basi tutamkamata afisa huyo na kumshtaki mahakamani,” Bw Kiboro
Mwaniki, afisa mkuu wa upelelelezi wa makosa ya jinai alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!