
Mvulana mmoja ambaye ni mtahiniwa a mtihani wa
kitaifa wa KCSE mwaka huu katika kaunti ya Bomet ametiwa mbaroni baada ya
kushukiwa kumlawiti mvulana wa miaka 7.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya kustaajabisha, mvulana
huyo mwenye umri wa miaka 19 anadaiwa kumhandaa mvulana wa miaka 7 kwa
peremende na soda kabla ya kumtendea unyama huo.
Citizen wanaripoti kwamba kamanda wa polisi wa kaunti
ndogo ya Konoin, alithibitisha kisa hicho akisema mshukiwa aliripotiwa
kutekeleza kitendo hicho kiovu kwa nyakati tofauti kabla ya kukamatwa.
"Ni tukio la kusikitisha na tunafanya kila
linalowezekana ili kupata kiini cha suala hilo, haki za watoto zilindwe kwa
gharama yoyote. Tunatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zaidi atusaidie katika
uchunguzi," kamanda huyo wa polisi alinukuliwa.
Inaarifiwa kwamba hii si mara ya kwanza kwa mvulana
huyo kufanya kitendo hicho cha ukatili kwa mtoto huyo, kila mara akimhadaa kwa
pipi na soda.
Mshukiwa huyo atakuwa anafanya mtihani wake wa KCSE
chini ya ulinzi mkali korokoroni.
Mitihani ya KCSE ilianza mapema wiki jana na tayari
vvisa kadhaa vya utovu wa kimaadili vimeripotiwa kando na visa vya wizi wa
mtihani huo.
Wikendi iliyopita, wavulana kadhaa wa shule ya
sekondari ya Shiners jijini Nakuru walitiwa mbaroni baada ya kudaiwa kuhusika
katika mauaji ya mtahiniwa mwenzao shuleni.
Kwa mujibu wa taarifa, wavulana hao mmoja wao
alimchoma mwenzao kisu tumboni hadi kufa baada ya mfarakano wa kuibiwa baadhi
ya vitu vyao kwenye bweni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!