
Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zambia, Harry Kalaba wa chama cha Citizens First amedai kuwa wananchi wengi wamegeukia kula misibani kutokana na gharama ya juu ya kumudu chakula nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa toleo la Daily Revelation, mwanasiasa huyo alitoa kauli hiyo akilenga kuikashifu serikali ya chama tawala cha UPND kikiongozwa na rais wa sasa Hachilema Hakainde kwa kile alisema ni kushindwa kupunguza gharama ya maisha kwa mwananchi wa kawaida.
Na Kalaba alisema serikali ya UPND itashindwa katika uchaguzi nchi nzima kwa sababu wameshindwa kutawala.
Zambia wanaelekea katika uchaguzi mkuu Agosti mwaka 2026.
Kiongozi huyo alizungumza hayo katika kituo kimoja cha redio nchini humo akisema jambo pekee ambalo serikali ya UPND ilifanya ni kugawanya nchi.
"Wazambia hawajawahi kuona aina ya ufujaji wa mizigo ambayo nchi inapitia hivi sasa. Rais Hakainde Hichilema alikuwa anaandika fomula ubaoni, sasa iko wapi hiyo formula ya kupunguza bei ya mafuta?”
Kalaba alisema Wazambia hawajawahi kuona viwango vya umaskini ambavyo nchi inakabili kwa sasa hivyo baadhi ya watu wamekimbilia kwenye nyumba za mazishi ili kupata chakula kwa sababu ya gharama kubwa ya maisha.
Hakainde aliibuka mshindi katika uchaguzi wa 2021 akimshinda aliyekuwa rais kiindi hicho, Edgar Lungu ambaye pia anataka kurejea katika uongozi wa taifa hilo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!