Mahakama katika Jiji la Masaka, Uganda ya Kati, imemhukumu mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 34 kifungo cha miaka 35 jela kwa kumlisha kinyesi na mkojo mtoto wa jirani yake mwenye umri wa miezi 10, katika kesi ambayo imeshangaza wengi.


Tukio hilo lilibainika baada ya video ya kitendo hicho kusambaa na kusababisha majirani waliohusika kuwaarifu viongozi ambao walimkamata mshukiwa.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, upande wa mashtaka, ukiongozwa na George Kalinaki, ulieleza kwa kina matukio ya tarehe 4 Novemba.


 


Ushahidi huo wa video, ambao ulisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii, ulionyesha mwanamke huyo akimlisha kinyesi kwa nguvu mtoto wa rafiki yake katika kile kilichoonekana kuwa kitendo cha ukatili wa kimakusudi.


 


Kufuatia tukio hilo, mtoto huyo alipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, jambo ambalo lilibaini jeraha lililopona kwenye jicho lake la kushoto, ishara ya unyanyasaji wa awali wa kimwili.


Mwendesha mashtaka pia aliieleza mahakama kuwa mwanamke huyo alipimwa na kukutwa na HIV, ingawa hii haikuathiri moja kwa moja hukumu hiyo.


Mwanamke huyo, ambaye alikiri makosa yake, alijaribu kukata rufaa kwa mahakama, akisema haelewi ni nini kilimsukuma kufanya kitendo kama hicho.


 


“Ibaadah yako, nakuomba unisamehe kwa matendo yangu. Naomba unipe hukumu kulingana na nilichofanya,” alisema huku akionyesha majuto. Walakini, ombi lake la kuhurumiwa halikusaidia sana uamuzi wa mahakama


Katika jibu thabiti, Hakimu Mkuu Aloysius Natwijuka alilaani vitendo vya Namwanje kama "vibaya na vya kishenzi," akibainisha kuwa tabia yake ilimtia alama kuwa hafai kwa jamii.


 


Akisisitiza haja ya kuwalinda watoto wa Uganda walio katika mazingira magumu, Natwijuka alisema, "Vitendo vya mfungwa vilikuwa vikubwa na vya kinyama, na hastahili kuonewa huruma. Ninakubaliana na serikali kwamba kuna haja ya kuwalinda watoto wadogo wasio na hatia kutoka kwa watu kama mfungwa. Kuna watu wengi huko nje ambao hufanya vivyo hivyo kwa watoto wasio na hatia lakini wanaenda bure.


 


Ingawa hakimu alikiri kuwa mwanamke huyo alikuwa mkosaji kwa mara ya kwanza na alionyesha kujutia, alishikilia kuwa kifungo cha muda mrefu gerezani ni muhimu kama funzo.