LGBTQ

MAHAKAMA ya Upeo nchini Uingereza imetangaza kuwa ufafanuzi wa mwanamke unatokana na jinsia ya kibaolojia katika uamuzi uliotajwa kuwa wa kihistoria katika taifa hilo. 

Lord Hodge alisema kuwa majaji watano wa Mahakama ya Upeo waliamua kwa kauli moja kwamba 'maneno mwanamke na jinsia katika Sheria ya Usawa yanarejelea 'mwanamke wa kibaolojia na jinsia ya kibaolojia'.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa sheria bado inawapa watu waliobadili jinsia ulinzi dhidi ya ubaguzi.

Katika uamuzi wa kurasa 88, majaji walisema: 'Ufafanuzi wa jinsia katika Sheria ya Usawa wa 2010 unaweka wazi kwamba dhana ya jinsia haina maana, mtu ni mwanamke au mwanaume.'

Uamuzi huo unaweza kuwa na athari kubwa juu ya jinsi haki za kijinsia zinavyotumika, pamoja na jinsi nafasi za wanawake pekee zinaruhusiwa kufanya kazi haswa katika taifa hilo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Uamuzi huo unaashiria hitimisho la vita vya kisheria vya muda mrefu kati ya serikali ya Uskoti na kikundi cha wanawake kuhusu ufafanuzi wa 'mwanamke' katika sheria ya Uskoti inayoamuru asilimia 50 ya uwakilishi wa wanawake kwenye bodi za umma.

Kesi hiyo ilihusu iwapo mtu aliye na cheti cha utambuzi wa kijinsia anayetambua jinsia yake kama mwanamke anafaa kuchukuliwa kama mwanamke chini ya Sheria ya Usawa ya 2010.

Serikali ya Uskoti ilisema kuwa watu kama hao wana haki ya kulindwa kulingana na jinsia, wakati kikundi cha kampeni cha For Women Scotland (FWS) kilidai kuwa inafaa kutumika kwa watu ambao wamezaliwa wakiwa wanawake pekee.

Akitoa uamuzi wa mahakama, Lord Hodge alisema: ‘Uamuzi wa pamoja wa mahakama hii ni kwamba maneno ‘mwanamke’ na ‘jinsia’ katika Sheria ya Usawa ya 2010 yanarejelea mwanamke wa kibaolojia na jinsia ya kibayolojia.’

Hukumu hiyo ilisherehekewa na mashirika ya kutetea haki za wanawake, ambao walishangilia nje ya mahakama, walifungua chupa ya shampeni na kuvunja wimbo baada ya uamuzi huo kutolewa.