Mwanaharakati wa kisiasa wa kizazi cha Gen Z, Kasmuel McOure amejiunga na chama cha ODM na kueleza sababu ya uamuzi huo ambao umewashangaza baadhi ya vijana wenzake.


Akizungumza wakati wa kukaribishwa rasmi chamani na gavana wa Homabay Gladys Wanga ambaye ni mmoja wa viongozi wa chama hicho, McOure alisema kwamba ODM ndicho chama cha sasa na cha kizazi kijacho.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mwanaharakati huyo aliyejizolea umaarufu wakati wa maandamano ya Gen Z alisema kwamba chama cha ODM kwa muda mrefu kimeonyesha ukakamavu wake katika mitihani migumu ya kidemokrasia na hivyo kukifanya kuwa chama pendwa.


Kijana huyo aliweka wazi kwamba chama cha ODM ni cha kila Mkenya, huku akiahidi kujitoa kwa hali na mali kuzunguka kote kuhakikisha amewasajili Wakenya wote chamani humo, haswa vijana wenzake.


“Tunaambia kila mtu mwenye akili timilifu kwamba tutatonga nje kwa nguvu zote kuwasajili vijana, sio tu wale wenye elimu lakini pia wale wasiokuwa na elimu, wale waalio katika taasisi zote za masomo, na kuhakikisha kwamba hiki ndicho chama.”


“Na kusema kweli kila Mkenya ni mwanachama wa ODM, amini kauli yangu, ndio maana ninasema tutajitoa kwa nguvu zote kuwasajili vijana ili kuwaleta katika chama cha sasa na baadae,” alisema.


McOure alimshukuru gavana Wanga kwa kumkaribisha chamani na kumhakikishia kwamba atakuwa sura ya vijana katika chama hicho kikongwe.


“Ikiwa uko tayari kujiunga na vuguvugu kubwa la kisiasa kwa ajili ya Kenya yenye haki, ya kidemokrasia ambapo kila mtu anaweza kuishi kwa heshima, zingatia @TheODMparty -chama kikubwa zaidi cha wafuasi katika Afrika Mashariki na Kati! Tunafufua Ligi za Vijana na Wanafunzi na tunatoa wito kwa vijana wa Kenya walio na shauku kusaidia kuunda maisha yetu ya baadaye. Simama nasi! Asante, mwenyekiti wa chama @gladyswanga, kwa imani yako na kutukaribisha wikendi hii,” alisema.