Polisi wamewaokoa raia 65 wa Ethiopia kutoka katika nyumba moja huko Mihang’o, Nairobi, ambapo walikutwa wakiwa wamedhoofika sana. Ugunduzi huo ulifanyika mapema jana baada ya msimamizi wa nyumba kuripoti kuona raia wa kigeni ndani ya nyumba hiyo, jambo lililopelekea maafisa kutoka kituo cha polisi cha Mihang’o kufika eneo hilo. Haijabainika wazi ni kwa muda gani walikuwa wamekaa hapo, lakini wakaazi wa eneo hilo walisema wamekuwa wakiwaona wageni hao kwa takriban wiki moja.