Watetezi wa haki wanatoa wito wa kuwepo kwa sheria maalum ya kuwalinda wazee dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji. Mwanzilishi wa shirika la Suqoon Kenya, Shakira Khawaja, anasema nchi hii inahitaji pia takwimu bora ili kusaidia katika kuandaa sera na programu zinazowalenga wazee. Aidha, anaihimiza serikali kupitia upya kigezo cha umri wa miaka 70 katika mpango wa 'Inua Jamii' ili kuwafikia na kuwasaidia wazee wengi zaidi. Leo ni Siku ya Kimataifa ya Wazee.

SHAKIRA KHAWAJA - GAPS