Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula anatoa wito kwa nchi za Afrika kutunga sheria kali dhidi ya wachafuzi wa hali ya hewa na kuanzisha ufadhili endelevu kwa ajili ya hatua za kukabiliana na hali ya hewa. Akizungumza wakati wa mkutano na wabunge wa Bunge la Afrika jijini Nairobi, Wetang’ula alipendekeza kutoza ushuru uchimbaji wa madini ili kufadhili ulinzi wa mazingira. Anasema Afrika lazima iungane katika kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa, akionya kwamba mifumo ya hali ya hewa isiyotabirika na mito inayokauka inazidi kuathiri jamii kote barani.