Gavana wa Kaunti ya Machakos, Wavinya Ndeti, ameahidi kuendeleza juhudi za kuongeza upatikanaji wa maji kote katika kaunti hiyo kwa matumizi ya nyumbani na kilimo kidogo. Akizungumza huko Mwala, Wavinya alifichua kuwa serikali yake inaendelea na ujenzi na uboreshaji wa mabwawa zaidi ya 30 kote katika Kaunti ya Machakos. Hatua hii, alisema, itahakikisha wakaazi wanapata maji ya uhakika kwa mahitaji yao ya nyumbani huku ikisaidia shughuli za kilimo.

WAVINYA NDETI - FERTILE