Rais William Ruto amewahimiza Wakenya wenye uwezo wa kifedha kununua hisa katika mradi uliopangwa wa Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Dangote East Africa huko Lamu, akisema mradi huo utawapa wananchi fursa ya kumiliki sehemu ya uwekezaji mkubwa wa kikanda. Akizungumza mjini Lamu, Ruto alisema serikali itakuwa na hisa katika mradi huo wenye thamani ya Sh trilioni 2, huku Wakenya wa kawaida wakiruhusiwa kununua hisa kupitia Soko la Hisa la Nairobi.
WILLIAM RUTO - SHARES