Rais William Ruto ametoa rambirambi kufuatia kifo cha mfanyabiashara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, akimtaja kama rafiki wa karibu baada ya kufariki katika ajali ya helikopta nchini Zimbabwe. Rais alizungumzia uhusiano wake binafsi na Chivayo, ambaye ziara zake za mara kwa mara nchini Kenya zilifanya urafiki wao uonekane wazi zaidi mwaka huu. Chivayo alionekana na Ruto katika matukio kadhaa, ikiwemo mikutano katika Ikulu na ziara katika makaazi binafsi ya Rais huko Kilgoris.