Rais William Ruto amemwomba Bilionea Aliko Dangote kuheshimu tarehe yake ya mwisho ya miezi 40 ya kukamilisha kiwanda cha kusafisha mafuta cha Lamu cha Sh trilioni 2.2. Akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi wa kiwanda hicho huko Lamu, Ruto alisema Wakenya watafuatilia kwa karibu ratiba hiyo baada ya Dangote kuahidi kurudi katika miezi 40 ijayo kufungua kiwanda hicho rasmi. Alibaini kuwa Wakenya wamezoea kuwawajibisha viongozi kwa ratiba za miradi zilizotangazwa.

WILLIAM RUTO - DATA