Rais William Ruto anatarajiwa leo kuweka jiwe la msingi la mabweni ya wanafunzi katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Shanzu, kabla ya kuelekea Tononoka kuzindua ujenzi wa mradi wa nyumba za bei nafuu. Mradi huo wa nyumba ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa nyumba unaolenga kuongeza upatikanaji wa makaazi mijini. Rais pia atakagua kituo cha abiria cha kivuko cha Likoni, kiungo muhimu cha usafiri kinachohudumia maelfu ya wasafiri kati ya Kisiwa cha Mombasa na bara kila siku.