Rais William Ruto angeshinda urais iwapo uchaguzi ungefanyika leo, kulingana na utafiti mpya uliofanywa na Politrack Africa. Rais Ruto anaongoza kwa asilimia 45.1, akifuatiwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna mwenye asilimia 19.6 na kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, mwenye asilimia 10.3. Utafiti huo, uliofanyika kati ya tarehe 15 na 25 Septemba ukihusisha washiriki 20,419, unamuweka kiongozi wa chama cha Jubilee, Fred Matiang’i, katika nafasi ya nne kwa asilimia 8.4, huku kiongozi wa DCP, Rigathi Gachagua, akifuata katika nafasi ya tano kwa asilimia 7.2.