Kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, amesema kuwa upinzani unakaribisha uwekezaji wa kigeni nchini Kenya lakini utaendelea kusisitiza kufuatwa kwa taratibu sahihi katika miradi mikubwa ili kuhakikisha inalinda maslahi ya taifa na wananchi wake. Kalonzo alisema kuwa kukosoa uwekezaji hakupaswi kuchukuliwa kama kupinga mtaji wa kigeni, akisisitiza kuwa ni lazima Wakenya wachunguze kwa kina mikataba mikubwa ili kuhakikisha kuna uwazi na kwamba miradi hiyo inaleta manufaa kwa umma.
KALONZO MUSYOKA - WELCOME