Mbunge wa Saboti, Caleb Amisi, anasema majina ya 'Linda' na 'Ukombozi' yalikuwa tayari yamesajiliwa kama majina ya vyama vya kisiasa kabla ya timu ya Edwin Sifuna kujaribu kuyatumia. Akizungumza katika Radio Jambo, Amisi alikanusha madai kuwa usajili huo ulifanywa kwa misingi ya kisiasa au kwa lengo la kukwamisha mipango ya kisiasa ya Sifuna. Kauli yake inafuatia uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kukataa ombi la Sifuna la kutumia majina hayo mawili kwa ajili ya chama chake cha kisiasa.

CALEB AMISI –NAMES