Baadhi ya wabunge wa UDA wamepuuza kutawazwa kwa Naibu Rais Kithure Kindiki kama mfalme na msemaji wa Mt Kenya, wakisisitiza kwamba joho la uongozi wa eneo hilo bado ni la Rais wa zamani Uhuru Kenyatta. Mbunge wa Ndia George Kariuki, mwenzake wa Juja George Koimburi na Mbunge wa Ndaragwa George Gachagua walisema sherehe hiyo, iliyofanyika katika Uwanja wa Kirigiti katika Kaunti ya Kiambu wiki moja iliyopita, haikuhusisha wazee wote na ilikosa baraka za jamii.
VOX POP – REJECT