Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) limethibitisha kuwa uwanja wa Allianz Arena wa klabu ya Bayern Munich utaandaa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ya mwaka 2028. Tangazo hilo lilitolewa jana na kamati tendaji ya UEFA, huku uwanja huo wa mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich, ukichaguliwa baada ya mchakato wa kuwania nafasi hiyo. Hii itakuwa fainali ya tatu ya Ligi ya Mabingwa kufanyika katika uwanja wa Allianz Arena, ambao pia uliandaa mechi hiyo kubwa ya soka la klabu barani Ulaya mwaka 2012 na 2025. Wakati huo huo, uwanja wa Camp Nou wa Barcelona utaandaa fainali ya mwaka 2029.

 

Philippe Coutinho amejiunga na rafiki yake wa karibu na mwenzake katika timu ya taifa ya Brazil, Neymar, katika klabu ya Santos FC hadi mwisho wa msimu. Santos ilimkaribisha mchezaji huyo kwenye mitandao ya kijamii kwa kuchapisha picha ya zamani ya Coutinho na Neymar wakiwa vijana wadogo, pamoja na picha mpya inayowaonyesha wakirudia pozi hilo wakiwa gym. Coutinho alianza taaluma yake ya soka katika klabu ya Vasco kabla ya kujiunga na Inter Milan na baadaye Liverpool mwaka 2013. Alihamia Barcelona kwa ada ya pauni milioni 142 mwaka 2018, na pia aliwahi kuchezea klabu za Bayern Munich, Aston Villa na Al-Duhail.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.