Rais William Ruto amepongeza hatua ya Nairobi kufanikiwa katika ombi lake la kuandaa Mashindano ya Dunia ya Riadha ya mwaka 2029. Ruto anasema huu ni wakati wa fahari na utukufu kwa Kenya na Afrika, na ni ushindi kwa vizazi vya wanariadha walioiletea Kenya sifa kwa umahiri wao katika mashindano ya uwanjani, barabarani na mbio za nyika. Kenya inakuwa taifa la kwanza barani Afrika kuandaa mashindano haya ya hadhi ya juu, ikiwa hapo awali iliwahi kuandaa Mashindano ya Dunia ya Riadha ya Nyika, Mashindano ya Dunia ya Vijana (chini ya umri wa miaka 18) na Mashindano ya Dunia ya Vijana (chini ya umri wa miaka 20).




Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Gilgil, Nakuru na Nyahururu.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.