Rais William Ruto amemtaka Gavana wa Siaya James Orengo kuacha kutumiwa na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kupinga mipango ya serikali, na badala yake awahudumie wananchi wa Siaya. Rais alisema kuwa wananchi wa Siaya hawakumchagua kuwa Gavana ili awe kibaraka wa Rais wa mstaafu. Aliongeza kuwa Uhuru ameshusha hadhi yake na kuwa kama kiongozi wa upinzani, ambaye amewashirikisha viongozi wengine kupinga miradi ambayo yeye mwenyewe alishindwa kuitekeleza alipokuwa madarakani.
WILLIAM RUTO - ORENGO