Kiongozi wa chama cha People's Party, Ndindi Nyoro, amekaribisha uamuzi wa jopo la majaji watatu uliotupilia mbali uuzaji wa hisa za serikali zenye thamani ya asilimia 15 katika kampuni ya Safaricom, akielezea hatua hiyo kuwa kinyume cha katiba. Akizungumza huko Kajiado wakati wa mazungumzo na wazee wa jamii ya Maasai, Nyoro alisema hisa hizo zinapaswa kurejeshwa mikononi mwa serikali kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama Kuu. Aidha, ameitaka serikali kusitisha uuzaji wa mali za umma bila kuwapa Wakenya fursa ya kushiriki katika mchakato huo.

NDINDI NYORO - MATAMSHI