Mwanamke mwenye umri wa miaka 18 amekamatwa baada ya polisi kufichua mpango unaodaiwa kuwa wa kutoroka gerezani katika Kituo cha Polisi cha Ruai. Christine Gitau alikuwa amepeleka chakula kwa washukiwa watatu wanaozuiliwa kituoni humo wakati maafisa walipogundua koleo na mkasi wa kukatia vyuma vilivyofichwa ndani ya chakula hicho. Washukiwa hao, wanakabiliwa na mashtaka ya wizi wa mabavu na ubakaji wa kundi. Polisi wanaamini kuwa vifaa hivyo vilikusudiwa kuwasaidia kutoroka.