Msichana mwenye umri wa miaka 11 amezama katika Mto Yala wakati akichota maji na marafiki zake katika Kijiji cha Kosoro, Kaunti Ndogo ya Gem Yala, Kaunti ya Siaya. Polisi wamebaini kuwa marehemu alikuwa mwanafunzi wa Darasa la Tano katika Shule ya Msingi ya Yala Township Comprehensive. Maafisa wa polisi walifika eneo la tukio na kubaini kuwa msichana huyo alienda mtoni na marafiki zake kuchota maji wakati alipoteleza kwa bahati mbaya na kutumbukia mtoni.