Kundi la maseneta limeelezea wasiwasi wake kuhusu kutokuwepo kwa viongozi wanaoiunga mkono serikali, ambao wana jukumu la kuratibu shughuli za serikali katika Seneti. Wakiongozwa na Seneta wa Kakamega, Boni Khalwale, maseneta hao walielezea hali hiyo ya kutokuwepo kwa viongozi hao kuwa ya kusikitisha na ishara ya uongozi duni. Walisema kuwa kutokuwepo kwao ni jambo la kutia wasiwasi hasa kwa kuzingatia kuwa Mawaziri kadhaa wanafika mbele ya Seneti kujibu maswali kuhusu wizara zao.


VOX POP-ABSENT