Rais wa LSK, Charles Kanjama, amesisitiza umuhimu wa kushughulikia changamoto za ndani ya sehemu za kazi katika sekta ya sheria. Akizungumza katika Kongamano na Maonyesho ya Mwaka kuhusu Ajira na Mahusiano ya Kazi katika Chuo Kikuu cha Strathmore, Kanjama alibaini kuwa kampuni nyingi za sheria ziko nyuma katika kutoa haki na kinga za msingi, kama vile mikataba ya ajira iliyoandikwa na likizo ya uzazi. Alisema kuwa LSK imedhamiria kusimamia utekelezaji wa viwango vya chini ili kuhakikisha kuwepo kwa taratibu za haki za ajira, kwa wote.
CHARLES KANJAMA – CONDITIONS