Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amemtetea Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kufuatia mashambulizi kutoka kwa Rais William Ruto, ambaye amemtuhumu kwa kufadhili upinzani. Gachagua alisema kuwa Ruto alichaguliwa licha ya Uhuru kupinga kugombea kwake, kwa sababu Uhuru alishindwa kuwashawishi Wakenya kumkataa, ingawa kufanya hivyo ndiyo ilikuwa hatua sahihi. Aidha, Gachagua alimkumbusha Ruto kuwa Uhuru si mpinzani wake katika uchaguzi wa mwaka 2027, bali ni wananchi wa Kenya.