Katibu wa Kilimo, Paul Rono, amesisitiza tena ahadi ya Kenya ya kuimarisha mifumo ya ubora wa mbegu na afya ya mimea ili kuongeza tija, kujenga uwezo wa kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa na kufungua fursa zaidi za masoko kwa wakulima. Alitoa kauli hiyo wakati akifungua warsha ya kimataifa kuhusu ubora wa mbegu na mifumo ya usalama wa afya ya mimea katika makao makuu ya KEPHIS huko Karen. Haya yanajiri huku maafisa wa KEPHIS wakiendelea kushinikiza kuwepo kwa adhabu kali zaidi dhidi ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa ghushi.


PAUL RONO - ELABORATE