Rais William Ruto anasema serikali itanunua feri za umma ili kuboresha usafiri katika ziwa Victoria na Turkana. Ruto alisema feri zilizopo Ziwa Victoria zinamilikiwa na watu binafsi, jambo linalofanya kuwe na haja ya kuwa na vyombo vya usafiri vinavyoendeshwa na serikali. Alisema mkakati kama huo utatumika katika Ziwa Turkana ili kurahisisha usafiri kati ya Turkana na kaunti jirani, ikiwemo Marsabit.
WILLIAM RUTO - FERRY