Mkutano wa 'Linda Mwananchi' unaashiria mabadiliko ya kizazi yanayoibuka katika siasa za Kenya. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Fanyamambo Kinuthia anasema kuwa vijana wa kizazi cha 'Gen Z' na wale wa kizazi cha 'millennials' wanazidi kudai fursa za uongozi, akibaini kuwa serikali ijayo inaweza kuwa na viongozi kutoka kizazi chao. Pia anasema mkutano huo ulionyesha kuwa Wakenya wanazidi kuzingatia zaidi misingi ya kisiasa, sera na viongozi binafsi, badala ya kushawishiwa na pesa au vishawishi vya mali kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027.

FANYAMAMBO KINUTHIA -TOMORROW