Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Mohammed Noor amewaagiza Machifu na Wasaidizi wa Machifu kote katika Kaunti hiyo kuimarisha ushirikiano na wakaazi kuhusu maandalizi ya mafuriko, akionya kwamba mitaro ya maji iliyoziba inaweza kusababisha maji ya mafuriko kurudi majumbani mara tu mvua itakapozidi kunyesha. Noor alisema wakaazi lazima waache kutupa taka kwenye mitari hii na kuhakikisha kwamba maji yanaweza kutiririka kwa uhuru ndani ya bahari katika kila eneo, bila majengo au kuta haramu zinazozuia njia yake.