Tume ya IEBC imetuliza hofu kuhusu kuchelewa kwa mchakato wa ununuzi wa teknolojia ya uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao, ikisema ina muda wa kutosha kukamilisha mchakato huo na kufanyia majaribio mifumo hiyo, kabla ya siku ya kupiga kura. Kamishna Alutalala Mukhwana anasema tume hiyo ina takriban siku 120 za kukamilisha ununuzi, zikifuatiwa na siku nyingine 60 kwa ajili ya majaribio ya uendeshaji na ukaguzi wa mifumo. Alikiri kuwa baadhi ya maamuzi ya ununuzi yalifikishwa mahakamani, lakini akasema tume hiyo iko tayari kutii maagizo yaliyotolewa na Mahakama.
ALUTALALA MUKHWANA - DAYS