Shirika la umoja wa mataifa la watoto UNICEF linatoa wito wa uwekezaji wa haraka katika hatua muhimu za kulinda watoto huku mvua za El Niño ikikaribia, ikionya kwamba zaidi ya watoto milioni 162 Mashariki na Kusini mwa Afrika wanakabiliwa na hatari kubwa kutokana na mishtuko inayohusiana na hali ya hewa. Mkurugenzi wa Kanda wa UNICEF wa Mashariki na Kusini mwa Afrika Etleva Kadilli alisema hatari kwa watoto zinaongezeka kadri hali ya hewa inavyozidi kuongezeka, na kutishia lishe, afya, elimu, usalama na upatikanaji wa maji salama na usafi wa mazingira.