Wizara ya Fedha imekosolewa kwa ufadhili mdogo wa taasisi za TVET nchini, licha ya Bunge kuongeza mgao wa taasisi hizi. Akiwa mbele ya Kamati ya Elimu ya Bunge, Katibu wa TVET Esther Muoria alisema kwamba idara hiyo haijapokea mgao wake kamili wa bajeti tangu mwaka 2023—hali ambayo imeathiri vibaya utoaji wa huduma katika taasisi za TVET. Kamati hiyo inatarajiwa kumwita Waziri wa fedha kujibu suala hilo.


ESTHER MUORIA - BUDGET