Viongozi wa upinzani wanaongeza juhudi za kuimarisha uungwaji mkono katika sehemu tofauti za nchi leo. Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka anatarajiwa Malindi, Kaunti ya Kilifi, huku Naibu Kiongozi wa Chama cha Jubilee Fred Matiang’i akitarajiwa kuzuru kaunti za Bomet na Narok. Kundi la Linda Mwananchi kwa upande mwingine linajiandaa kwa mkutano wa hadhara wa Homa Bay wikendi hii.