AFC Leopards watawakaribisha KCCA FC ya Uganda katika mechi ya kirafiki kesho, katika Uwanja wa Ulinzi Sports Complex wanapokamilisha maandalizi yao ya msimu, kabla ya kuanza kwa msimu wa KPL 2026/27. Mechi hiyo itampa kocha mkuu wa Leopards, Fred Ambani fursa ya kuwatazama wachezaji wake wapya waliosajiliwa na kujaribu mifumo tofauti. Ingwe iliwashinda wapinzani wao wa ndani Kakamega Homeboyz 2-0 katika mechi nyingine ya kirafiki Jumatano, baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Ligi ya Tanzania Pamba Jiji FC jijini Dar er Salaa, Jumapili.


 

Msururu wa Kitaifa wa Sportpesa Sevens unarejea wikendi hii huku Kabeberi Sevens ikiangaziwa katika uwanja vya RFUEA, wikendi hii. Mabingwa KCB wataanza utetezi wao wa taji dhidi ya wapinzani wao Kabras Sugar, Chuo Kikuu cha Masinde Muliro na Nakuru RFC katika kundi D, huku Kenya Harlequins, Daystar Falcons, Kisumu RFC na Impala wakicheza pamoja katika kundi A. Kundi B lina Mwamba, Strathmore, Nondies na Catholic Monks, huku Menengai Oilers, Zetech Oaks, Blak Blad na Mombasa RFC zikimaliza katika kundi D.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Kajiado na Narok.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.