Raia wawili wa India waliotekwa nyara muda mfupi baada ya kufika JKIA wameokolewa, huku raia watatu wa Pakistani wanaoshukiwa kuwashika mateka wamekamatwa. Waathiriwa, Sandeep Sandeep na Ishwar Singh, waliokolewa kutoka kwenye nyumba ndogo katika eneo la Tumaini Estate, Nkoroi, Kajiado South, ambapo wapelelezi waliwakuta wamefungwa. Polisi wanasema washukiwa walikuwa wamedai dola elfu 32 za Marekani kama fidia kutoka kwa familia za waathiriwa nchini India. Washukiwa hao watatu bado wako kizuizini.