Mteuliwa wa Tume ya Utumishi wa Umma Flora Mutua ametoa wito wa usimamizi imara wa orodha ya mishahara ili kushughulikia changamoto ya wafanyakazi hewa. Akiwa mbele ya Kamati ya leba wakati wa kukaguliwa kwake, Mutua alisema maafisa wanaohusika na kusimamia mishahara wanapaswa kuwajibishwa iwapo ukaguzi utabaini wafanyakazi hewa. Alisema kuimarisha mifumo ya mishahara kutasaidia kuzuia kupotea kwa fedha za umma kupitia rekodi za ajira za ulaghai au zisizo za kawaida.
FLORA MUTUA - PAYROLL