Naibu gavana wa Machakos Francis Mangangi, amepinga mkutano wa ruwaza ya mwaka 2060 wa rais William Ruto katika KICC. Akizungumza huko Kathiani, naibu gavana huyo alipuuza mpango huo kama mbinu ya kuwadanganya Wakenya ili wamchague mwaka ujao. Alitaja miradi muhimu iliyojumuishwa katika ruwaza ya Kibaki ya mwaka 2030 kama vile jiji la Konza na bwawa la Thwake miongoni mwa mingine mingi ambayo ilihitaji kukamilika kabla ya mradi mwingine wowote kuanza.
FRANCIS MWANGANGI - VISION