Mgomo wa maafisa wa kliniki umeingia siku yake ya 26, huku kaunti 29 kati ya 47 zikiwa zimetia saini Mkataba wa CBA na maafisa hao. Mwenyekiti wa muungano, Peterson Wachira, anasema hitaji kuu ni utekelezaji wa CBA, si utiaji saini wake, akiongeza kuwa ni kaunti 16 pekee kati ya 29 ndizo zilizowasilisha makubaliano hayo kwa SRC kwa barua ya kutopinga. Maafisa hao wanasema mgomo huo utaendelea hadi matakwa yao yatakaposhughulikiwa.


PETERSON WASHIRA – CBA