Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta kinafanya sherehe ya pamoja ya kuhitimu na Taasisi ya Sayansi ya Msingi, Teknolojia na Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Pan African katika chuo kikuu chake huko Juja hii leo. Zaidi ya wahitimu 5,0000 wanatarajiwa kupokea shahada, diploma na vyeti katika nyanja mbalimbali. Sherehe hiyo inaongozwa na Chansela wa JKUAT Profesa Joseph Ndung’u, huku Waziri wa Elimu Julius Ogamba akiwa Mgeni Rasmi.