Wapenzi wachanga wamefariki kwa kujitoa uhai huko Eldoret katika kile ambacho polisi wanashuku kuwa huenda ni malumbano ya kimapenzi. Tukio hilo lilitokea nyumbani kwao Sogomo, nje kidogo ya jiji la Eldoret, karibu na Chuo Kikuu cha Eldoret. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Uasin Gishu Wilberforce Sicharani alithibitisha tukio hilo, akisema mwanamke huyo, mwenye umri wa miaka 26, alikuwa mwalimu katika shule ya eneo hilo huku mwanaume huyo akiwa na umri wa miaka 32. Sicharani alisema polisi waliitwa nyumbani baada ya mwanaume huyo kupatikana akining'inia kwenye mti baada ya kujitia kitanzi.