Kushindwa kupima Virusi vya HIV au kuanza matibabu mapema kunaweza kuongeza hatari ya maambukizi na kuendelea hadi kukithiri kwa ugonjwa huo. Eric Mutua, Mkuu wa Ugavi na Usalama wa Bidhaa za HIV katika NASCOP, anasema HIV iliyokithiri inaweza kudhoofisha kinga na kuwaweka wagonjwa katika hatari ya kupata Kifua Kikuu, Kaposi’s sarcoma na cryptococcal meningitis, miongoni mwa magonjwa mengine. Anawasihi Wakenya kupima mara kwa mara na kuanza matibabu mara moja ikiwa watagunduliwa kuwa na virusi. 

ERIC MUTUA - HIV