Maendeleo Chap Chap itaunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais William Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa 2027, Waziri wa Leba Alfred Mutua ambaye anaongoza chama hicho amesema. Katika taarifa kufuatia mkutano wa Baraza la Uongozi la Kitaifa la chama hicho uliofanyika jana, Mutua hata hivyo alisema watawasimamisha wagombea katika viti vingine vya uchaguzi ikiwa ni pamoja na MCA, Mbunge, Mwakilishi wa Wanawake, Seneta na Gavana.