Huduma ya Usajili Katika Vyuo Vikuu nchini (KUCCPS) imefungua jukwaa la kutuma maombi ya usajili wa Septemba mwaka huu katika Chuo cha Ronald Ngala Utalii katika Kaunti ya Kilifi. Taasisi hiyo imewasihi wanafunzi wanaostahili watakaopenda kusomea kazi za ukarimu na utalii kuwasilisha maombi yao kupitia jukwaa la KUCCPS ifikapo tarehe 23, mwezi huu.  KUCCPS ilisema uandikishaji wa hivi karibuni unawapa wanafunzi fursa ya kujiandikisha katika programu 13 za diploma na cheti katika kampasi ya Kilifi.