Familia za Wakenya walioajiriwa kupigana katika vita vya Urusi na Ukraine zina wasiwasi kuhusu ukimya wa serikali kuhusu usaidizi unaotolewa kwa familia zilizoathiriwa. Msemaji Peter Kamau anasema serikali inapaswa kuonyesha waziwazi usaidizi inaodai kutoa, badala ya kufanya hivyo faraghani. Kamau anasema hii inazua shaka kuhusu jinsi kesi hizo zinavyoshughulikiwa, akisisitiza kwamba kuwasaidia Wakenya walioathiriwa haipaswi kuchukuliwa kama suala la kisiasa.

PETER KAMAU – HELP