Tume ya EACC na Mkutano wa Maaskofu Wakikatoliki wa Kenya wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wao ili kukuza uadilifu na kupambana na ufisadi. Kulingana na taarifa ya EACC iliyotolewa baada ya mkutano jijini Nairobi, maafisa wa EACC na ujumbe wa KCCB walisisitiza jukumu muhimu la mashirika ya kidini katika kuunda maadili na kuhamasisha jamii za watu wa mashinani. Taasisi zote mbili ziliahidi kushirikiana katika mipango ya uongozi wa maadili na utawala bora kote nchini.